Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA ilirusha chombo cha uchunguzi cha sayari zilizoko nje ya mfumo wa jua TESS tarehe 18 usiku. Chombo hiki kitafanya kazi baada ya darubini ya Kepler. Darubini hiyo ilirushwa angani mwaka 2009, na kupangwa kufanya kazi kwa miaka mitatu na nusu, ingawa bado inafanya kazi lakini ni vigumu kwa darubini hiyo kutafuta sayari nyingi zaidi.
Je, kwanini binadamu wanafanya kazi kubwa ya kutafuta sayari zilizoko nje ya mfumo wa jua?
Binadamu wanafanya hivyo ili kujibu maswali matatu.
Kwanza, asili yetu ni wapi? Kutafiti asili ya sayari na masuala husika ni kazi muhimu zaidi ya utafiti wa sayari zilizoko nje ya mfumo wa jua.
Pili, utamaduni wa binadamu ni wa pekee ulimwenguni? Baada ya kujua dunia si kiini cha ulimwengu, watu walianza kukisia kuwa huenda kuna viumbe na tamaduni nje ya dunia, lakini wanasayansi bado hawajapata ushahidi wa kuwepo kwa viumbe kwenye sayari za mfumo wa jua, hivyo walianza kutafiti sayari zilizoko nje ya mfumo huo.
Tatu, tutakwenda wapi? Hadithi nyingi za sayansi ya kubuni zinasema binadamu watakwenda sayari nyingine baada ya rasilimali za dunia kwisha, na sasa kutafuta sayari zinazofaa maisha ya viumbe kumekuwa utafiti rasmi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |