Watafiti wa Australia wamevumbua rasilimali mpya aina ya polymer (molekuli nyingi zilizoungana pamoja) ambayo inaweza kuvuta mafuta yaliyovuja baharini kama sponji.
Rasilimali hiyo iliyotengenezwa kwa mafuta machafu na salfa inaweza kuelea majini, baada ya kuvuta mafuta, inaweza kutumiwa tena baada ya kushinikizwa.
Dr. Justin Chalker kutoka Chuo Kikuu cha Flinders cha Asutralia amesema rasilimali hiyo inaweza kuondolewa kwa urahisi kwa nyavu baada ya kuvuta mafuta, hivyo itasaidia sana katika kuondoa mafuta kwenye bandari au fukweni. Na kama mafuta mengi yakivuja baharini, watu wanaweza kuiweka rasilimali hivyo kwenye mitambo ya kuchuja maji.
Dr. Chalker amesema mwanzoni watafiti walijaribu kutumia tena takataka za chakula na mafuta za viwandani, lakini waligundua kuwa rasilimali hiyo inafanya vizuri katika kuondoa mafuta na uchafuzi mwingine wa kikaboni.
Hivi sasa watafiti wanapanga kujenga kiwanda cha kuzalisha rasilimali hiyo kusini mwa Australia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |