• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa korea Kusini autaka Umoja wa Mataifa kufuatilia mpango wa Korea Kaskazini wa kufunga vituo vya majaribio ya nyuklia

    (GMT+08:00) 2018-05-01 18:13:13

    Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini ameutaka Umoja wa Mataifa kufuatilia mpango wa Korea Kaskazini wa kufunga vituo vyake vya majaribio ya nyuklia.

    Msemaji wa rais huyo Kim Eui-kyeom amesema, rais Moon alifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ambapo viongozi hao walibadilishana maoni kuhusu matokeo ya mkutano wa tatu wa kilele wa Korea uliofanyika wiki iliyopita. Rais Moon amemwambia Katibu Mkuu huyo kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameahidi kufanya wazi mchakato wa kufunga kituo cha majaribio ya nyuklia cha Punggye-ri kwa Korea Kusini na Marekani, na pia kwa jamii ya kimataifa.

    Kwa upande wake, Bw. Guterres amesema yuko tayari kutoa ushirikiano katika mchakato huo, huku akisema ingawa wito wa rais Moon unahitaji idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, atafanya juhudi kusaidia kumaliza mazungumzo ya amani kuhusu Peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako