• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la IS latangaza kuwajibika na shambulizi dhidi ya tume ya uchaguzi Libya

    (GMT+08:00) 2018-05-03 09:10:54

    Kundi la Islamic State limekiri kufanya shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya makao makuu ya tume ya uchaguzi ya Libya mjini Tripoli.

    Kundi hilo pia limesema shambulizi hilo linatokana na amri ya msemaji wa kundi hilo Abu Hassan al-Muhajir, na limesababisha vifo vya wanausalama na wafanyakazi zaidi ya 15 wa tume hiyo.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani shambulizi hilo la kigaidi, na kutoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na pole kwa majeruhi kwenye shambulizi hilo.

    Shambulizi hilo limetokea wakati serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa, kwa kushirikiana tume ya Umoja huo nchini Libya, inafanya maandalizi ya uchaguzi wa rais na wabunge kabla ya mwisho wa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako