• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa fedha kutoka China, Japan, na Korea Kusini wasisitiza kujizuia na vitendo vya kujilinda

    (GMT+08:00) 2018-05-04 17:45:42

    Mawaziri wa fedha na magavana wa Benki Kuu za China, Japan, na Korea Kusini wamesisitiza haja ya kuzuia aina zote za kujilinda, na kukubaliana kuhakikisha mfumo wa wazi wa biashara na uwekezaji wa pande nyingi.

    Nchi hizo tatu za kaskazini mashariki mwa Asia zimekutana kando ya mkutano wa 51 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Asia (ADB) unaofanyika Manilla, mji mkuu wa Philippines. Mkutano huo unalenga kujadili maendeleo ya sasa ya kiuchumi na uwezekano wa hatari katika soko la fedha na mazingira ya kiuchumi yaliyopo.

    Mawaziri hao pia wamepongeza Azimio la Panmunjeom lililofikiwa kati ya viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskazini April 27 mwaka huu, na kuongeza kuwa wanatarajia maendeleo zaidi katika kupunguza mvutano wa siasa za kijiografia katika eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako