Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA imesaini makubaliano na kampuni ya huduma za kuagiza teksi Uber, ili kutafiti teknolojia ya usafiri wa angani na kuanzisha mfumo salama na wenye ufanisi mkubwa wa usafiri wa angani katika miji yenye wakazi wengi.
Kwa mujibu wa makubaliano, kampuni ya Uber itaipatia NASA data zake kuhusu mtandao wa usafiri wa angani, na NASA itatathimini athari ya urukaji wa ndege ndogo juu ya miji kwa kutumia mfumo mpya wa usimamizi wa ndege. Ndege ndogo ni pamoja na ndege za mizigo zisizo na rubani na ndege zinazobeba abiria ambazo zinaweza kuruka wima.
NASA itafanya majaribio katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Fort Worth mjini Dallas, ili kutathimini suala la usalama wakati ndege ndogo inapopita eneo lenye ndege nyingi.
Maofisa husika wa NASA wanaona kuwa usafiri wa angani huenda utaleta mabadiliko makubwa kwa usafiri wa watu na usafirishaji wa mizigo mijini, na kubadilisha mtindo wa maisha yetu kama ilivyokuwa kwa simu za mkononi aina ya Smartphone.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |