• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Qatar yazuia uingizaji wa bidhaa kutoka UAE, Saudi Arabia, Bahrain na Misri baada ya mwaka mmoja wa kuwekewa vikwazo

    (GMT+08:00) 2018-05-28 17:57:57

    Qatar imesema itazuia bidhaa zinazotoka kwenye nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia, Bahrain na Misri, ikiwa ni karibia mwaka mmoja tangu nchi hizo nne kuiwekea vikwazo.

    Taarifa iliyotolewa na serikali ya Qatar imesema, ili kulinda usalama wa watumiaji nchini Qatar na kupambana na usafirishaji haramu wa bidhaa, serikali imetoa maelekezo ya kutafuta wasambazaji wapya wa bidhaa kadhaa zinazoathiriwa na hatua hiyo.

    Mwezi Juni mwaka jana, Saudi Arabia, Bahrain, UAE na Misri zilivunja uhusiano wa kidiplomasia na wa anga, bahari na ardhini na Qatar, zikiituhumu nchi hiyo yenye utajiri wa gesi kufadhili ugaidi na kushirikiana na Iran dhidi ya maslahi ya nchi za Kiarabu. Qatar imekana tuhuma hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako