Kikundi cha watafiti cha kimataifa kimegundua nyoka wa aina 5 wanaoweza kula konokono kwa taya na meno katika misitu ya mvua ya Amazon Amerika ya Kusini. Utafiti huo umetolewa hivi karibuni kwenye jarida la ZooKeys.
Watafiti kutoka Ecuador, Peru na Marekani wamefanya utafiti katika misitu hiyo kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2017, na kugundua nyoka hao wadogo.
Watafiti wamelinganisha magamba na DNA za nyoka hao na sampuli zaidi ya aina 200 zilizotambuliwa na kugundua kuwa nyoka hao ni wa aina mpya.
Dr. Alejandro Arteaga amesema nyoka hao wanaishi kwenye miti na hawana sumu, tofauti na nyoka wengine wanaopenda kula mijusi, vyura, ndege, panya na popo, nyoka hao wanategemea konokono, lakini hawali konokono kwa kuvuta miili yao kutoka kwenye magamba kama binadamu wanavyokula chaza, bali wanaingiza taya kwenye magamba ya konokono, halafu wanakuvuta miili ya konokono kwa meno yanayopinda, wanakula kwa kasi bila kuvunja magamba ya konokono.
Miongoni mwa nyoka hao wa aina 5, aina 4 wako hatarini. Watafiti wamependekeza kuweka aina 3 kwenye orodha ya viumbe waliko hatarini ya kutoweka ya IUCN.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |