Ofisi ya sera za sayansi na teknolojia ya Ikulu ya Marekani imetoa ripoti kuhusu mkakati wa kukabiliana na tishio sayari ndogo na nyota mkia zilizoko karibu na dunia katika miaka 10 ijayo. Ripoti hiyo imesisitiza kuwa siku hizi hakuna magimba ya angani yatakayotishia dunia.
Ripoti hiyo inasema ingawa ushirikiano wa kimataifa ni njia nzuri zaidi ya kukabiliana na tishio hilo, lakini Marekani pia itajaribu kufanya shughuli kwa kujitegemea wakati magimba ya angani yatakapoigonga dunia.
Sayari ndogo yenye kipenyo zaidi ya mita 140 itaathiri vibaya eneo fulani hata bara zima. Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA imekadiria kuwa kuna sayari elfu 25 za ukubwa huo angani, lakini nusu tu zitagunduliwa ifikapo mwaka 2033.
Ripoti hiyo pia inasema magimba ya angani yenye kipenyo cha mita 1000 hivi huenda yatasababisha matetemeko ya ardhi na tsunami. NASA imetambua mahali pa sayari zote zenye ukubwa huo, lakini nyota mkia zilizoko nje ya mfumo wa jua pia zinaweza kuiathiri dunia, na muda wa kutoa tahadhari utakuwa ni miezi kadhaa tu.
Ripoti hiyo imetoa malengo matano, yakiwemo kuinua uwezo wa kugundua na kuchunguza magimba hayo, uwezo wa kutoa tahadhari, na teknolojia ya kusukuma na kubomoa magimba hayo, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na kuanzisha kanuni za kukabiliana na hali ya dharura.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |