Kamera ya miali isiyoonekana chini ya upinde inaweza kupiga picha gizani, na ni chombo muhimu cha kijeshi. Watafiti wa Marekani wamesanifu rasilimali mpya ambayo inaweza kuwasaidia watu na vifaru kutotambuliwa na kamera hiyo.
Miali isiyoonekana chini ya upinde ni wimbi la sumaku umeme lenye masafa kati ya wimbi maikro na miali inayoonekana. Binadamu na injini za vifaru huwa zinatoa miali hiyo, na inaweza kutambuliwa na kamera maalum gizani au ukunguni. Watafiti wa tawi la Madison la Chuo Kikuu cha Wisconsin la Marekani wametoa ripoti kwenye jarida la Advanced Engineering Materials ikisema wamesanifu rasilimali yenye unene usiozidi milimita 1 ambayo inaweza kuvuta asilimia 94 ya miali isiyoonekana chini ya upinde. Vitu vikifunikwa na rasilimali hiyo, havitatambuliwa na kamera maalum.
Rasilimali hiyo imetengenezwa na silikoni nyeusi. Juu ya silikoni nyeusi kuna sindano nyingi nyembamba zinazosimama. Miali ikifika juu ya rasilimali hiyo, itarudishwa kati ya sindano hizi na ni vigumu kutoka, hivyo ni vigumu kwa rasilimali hiyo kugunduliwa. Watafiti wamechonga sehemu ya juu ya silikoni nyeusi kwa chembe ndogondogo za fedha, na kuzifanya sindano hizi ziwe nyembamba na ndefu zaidi, na kuongeza uwezo wa rasilimali hiyo wa kuvuta miali isiyoonekana chini ya upinde.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |