Filamu nyingi za sayansi ya kubuniwa inasimulia kuwa dinosaur aina ya Tyrannosaurus anapowinda mnyama mwingine, anafunua mdomo mkubwa, na kutoa ulimi wake nje ya mdomo. Lakini utafiti mpya uliofanywa na wanasayansi wa China na Marekani unaonesha kuwa jambo hili si kweli.
Utafiti uliotolewa kwenye jarida la PLoS One la Marekani unaonesha kuwa ulimi wa Tyrannosaurus huenda ni mfupi na mpana kama mamba mwenye mdomo mfupi, hivyo hakuweza kutoa ulimi wake nje ya mdomo.
Kikundi cha watafiti wa idara ya wanyama wenye uti wa mgongo na binadamu wa kale ya taasisi ya sayansi ya China Bw. Li Zhiheng wakitumia chombo cha kuchunguza vitu kwa miali ya X-ray cha tawi la Austin la Chuo Kikuu cha Texas cha Marekani, wamescan mifupa ya ulimi ya dinosaur, pterosaur, mwamba wenye mdomo mfupi na ndege wa kisasa.
Matokeo yanaonesha kuwa mifupa ya ulimi ya dinosaur wengi inafanana na ile ya mwamba mwenye mdomo mfupi, hivyo ndimi zao haziwezi kutolewa nje ya mdomo. Lakini pterosaur, dinosaur wanaofanana na ndege na ndege wa kisasa wana mifupa ya ulimi ya aina mbalimbali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |