Kikundi cha wanaakiolojia kimesema wamegundua ushahidi kwamba binadamu walianza kuoka mikate mapema zaidi kuliko kuanza shughuli za kilimo kwa miaka 4000.
Utafiti uliotolewa kwenye jarida la PNAS la Marekani unaonesha kuwa wanaakiolojia wamegundua mabaki ya mikate ya kuokwa yenye historia ya miaka elfu 14.4 katika maskani ya kale ya binadamu kaskazini mashariki mwa Jordan. Kabla ya hapo, ushahidi kuhusu bindamu kuoka mikate uligunduliwa nchini Uturuki ambao una historia ya miaka 9100.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen Denmark, Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Cambridge Uingereza wamegundua kuwa binadamu wa kale walisaga, kuchuja, kukanga na kupika nafaka pori, zikiwemo shayiri na ngano.
Watafiti wamesema ushahidi mpya unaonesha kuwa kuoka mikate kwa nafaka pori huenda kuliwahimiza binadamu wa kale kuanza kulima nafaka, na kuleta mapinduzi ya kilimo katika enzi ya zana mpya za mawe.
Kabla ya hapo, zana za mawe zenye umbo la mundu na zana za kusaga ziliwahi kugunduliwa huko, hivyo wanaakiolojia wameshakisia kuwa binadamu wa kale walijua njia nzuri ya kula nafaka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |