Utafiti mpya uliotolewa kwenye jarida la Uingereza la "The Lancet" umeonesha kuwa mwaka 2016 watu milioni mia 3 hivi wanabeba virusi vya Hepatitis B duniani.
Watafiti kutoka Marekani wametumia takwimu za tafiti za awali na maoni ya wataalamu wa nchi mbalimbali kujenga mfano wa utafiti na kugundua mwaka 2016 watu milioni 292 duniani wanabeba virusi vya Hepatitis B ambayo inachukua asilimia 4 ya watu wote duniani. Wengi wao wapo katika Asia ya Mashariki na sehemu iliyo kusini mwa jangwa la Sahara.
Ugonjwa wa Hepatitis B huambukizwa kupitia mama na watoto wachanga, damu au majimaji mengi ya mwili. Wanaoambukizwa virusi vya Hepatitis B ambao antijeni zao kwenye virusi hivyo vikionesha chanya kwa miezi zaidi ya 6 lakini uwezo wao wa ini bado uko katika kiwango cha kawaida wanaitwa wanaobeba virusi vya Hepatitis B, na baadhi yao wanakuwa wagonjwa wa Hepatitis.
Watafiti hao pia wamesema, hivi sasa hakuna dawa yoyote inayotibu Hepatitis, lakini dawa ya kupambana na virusi hivyo inaweza kupunguza ugonjwa huo. Kama watu hao hawatapata tiba, ugonjwa huo unaweza kuwa saratani ya ini. Takwimu zinaonesha kuwa watu laki sita hivi wamefariki kutokana na maradhi ya ini yanayosababishwa na ugonjwa wa Hepatitis.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |