Emmerson Mnangagwa ashinda uchaguzi Zimbabwe
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameshinda uchaguzi wa urais nchini Zimbabwe kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.
Katika majimbo 10 yote yalioyotangazwa, Mnangagwa ameshinda kwa asilimia 50.8 ya kura kwa asilimia 44.3 alizopata mgombea wa chama cha upinzani Nelson Chamise.
Polisi waliwaondoa upinzani wakati wa kutangazwa matokeo baada ya kukataa kuyakubali matokeo hayo.
Mwenyekiti wa chama cha MDC Alliance, Nelson Chamisa amesema kuhesabiwa kwa kura hakukufanyiwa uhakiki.
Kwa ushindi wa asilimia 50 wa Mnangagwa umesababisha aepuke kwenda duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya Chamisa.
Rais Mnangagwa amesema katika ukurasa wake wa Twitter kuwa huu ni mwamzo mpya.
Bwana Chamisa amesisitiza kuwa ZANU-PF haikushinda uchaguzi huu, wanajaribu tuu kupitisha suala lisilo na ukweli, amesema pia watapambana na suala hilo.
Uchaguzi huu ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kung'atuliwa madarakani.
Muungano wa Afrika, mapema wiki hii umesema kuwa uchagauzi huo ulikuwa huru na wa haki , na kuwa unaadhimisha wakati muhimu wa mabadiliko ya kisiasa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |