China yatoa msaada wa chakula kwa Afghanistan
Hafla ya kukabidhi msaada wa kibinadamu wa chakula kutoka China kwa Afghanistan imefanyika huko Kabul, na kuhudhuriwa na Balozi wa China nchini Afghanistan Bw. Liu Jinsong na Waziri wa Usimamizi wa Maafa na Mambo ya Kibinadamu wa Afghanstan Bw. Najib Aka Fahim.
Balozi Liu amesema msaada huo wa chakula unatolewa ili kuunga mkono juhudi za Waafghanistan katika kukabiliana na taabu, na pia kuonyesha urafiki mkubwa kati ya serikali na watu wa nchi hizo mbili.
Ameongeza kuwa kipindi kijacho China itafikiria kusaidia kujenga mfumo wa tahadhari ya maafa na kutoa vifaa vya misaada kwa Afghanistan, na kutarajia nchi hiyo itapata amani, utulivu na mafanikio mapema.
Waziri Fahim ameshukuru msaada wa China, na kusema Afghanistan inaahidi kusambaza chakula haraka iwezekanavyo kwa watu walioathirika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |