Tangu kufanyika kwa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2015, mjini Johannesburg, China imetekeleza kikamilifu mipango kumi ya ushirikiano kati yake na Afrika. Pia imetimiza ahadi yake ya kutoa msaada wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 60 kwa Afrika. Licha ya hayo, baadhi ya ujenzi wa reli, barabara, miundo mbinu na maeneo ya biashara umekamilika na mwingine bado unaendelea. Aidha, ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta za sayansi, elimu, utamaduni, afya, kuondoa umaskini na kuleta manufaa kwa watu bado unaendelea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |