• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Israel na Russia wazungumza tena kutokana na kutunguliwa kwa ndege ya Russia nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-09-25 09:29:31

    Waziri mkuu wa Israel Bw Benjamin Netanyahu ameongea kwa njia ya simu na rais Vladimir Putin wa Russia, na kuzungumza tena kuhusu tukio la ndege ya Russia kutunguliwa na mfumo wa makombora ya ulinzi wa anga wa Syria.

    Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imetoa taarifa ikisema Bw. Netanyahu anaamini ukweli wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Israel. Jeshi la Syria na majeshi ya Iran yaliyoko nchini Syria ndio wanawajibika na shambulizi hilo. Ameongeza kuwa Israel itaendelea kulinda usalama wake na maslahi yake kwenye Mashariki ya Kati.

    Rais Putin amesema Israel haikufuata makubaliano ya kupeana taarifa za matukio ya hatari kati ya Russia na Israel, na kusababisha tukio hilo. Ameitaka Israel ichukue hatua ili kuepusha kutokea tena kwa tukio kama hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako