Ubalozi wa China nchini Kenya umefanya sherehe mjini Nairobi, kuadhimisha miaka 69 tangu kuzinduliwa rasmi kwa Jamhuri ya Watu wa China. Kwenye hotuba aliyotoa kwenye sherehe hiyo, iliyosomwa kwa niaba yake na Bwana Li Xuhang wa ofisi ya mambo ya kigeni, Balozi Sun amesema China imepiga hatua za kuigwa na mataifa mengine duniani, kutokana na juhudi zake za miaka 40 iliyopita.
Sherehe hizo zimefanyika wakati uhusiano kati ya China na Kenya unaendelea vizuri, na kampuni 400 za Kichina zimewekeza na kuajiri wakenya zaidi ya 55,000, na miradi ya ushirikiano inayojengwa kwa ufadhili wa China kama wa SGR, ikiendelea kujengwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |