Kenya imeanzisha kampeni ya kuhimiza mafungamano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia mtandao wa Internet.
Katibu mkuu wa wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki na maendeleo ya kikanda ya Kenya Bibi Susan Koech, amesema kampeni hiyo iitwayo Ushirikiano Digital, itakuwa jukwaa la kidijitali la kubadilishana habari kati ya vijana wa vyuo vikuu na wizara hiyo.
Amesema kampeni hiyo itawasaidia vijana na umma kuelewa hadhi na mchakato wa mafungamano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesisitiza kuwa jumuiya ya Afrika Mashariki ni soko muhimu kwa bidhaa za Kenya, inatengeneza fursa kwa uwekezaji kati ya nchi wanachama, na pia inazisaidia nchi hizi kutoa sauti ya pamoja katika jumuiya ya kimataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |