Uganda yafanya maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru
Uganda wiki hii imefanya maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru kwa kuhimiza uzalishaji mali kwa kaya.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda alitoa hotuba kwa njia ya televisheni huko Kyotera, ambako yalifanyika maadhimisho ya kitaifa, akisema waganda wanatakiwa kufanya kilimo cha mazao ya chakula na biashara ili kuongeza kipato kwa familia.
Rais Museveni amesema Uganda inapaswa kubadili njia za kilimo kutoka kilimo cha kujikimu na kuwa kulimo cha kisasa. Amesema serikali itahakikisha inaweka mifumo ya umwagiliaji kwenye sehemu mbalimbali za nchi, ili kuhakikisha kuna maji ya kutosha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |