• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Kenya kufanya kongamano la kuhimiza nguvu ushindani kiviwanda

    (GMT+08:00) 2018-11-09 09:24:13

    Baraza la ushirikiano kuhusu kuhimiza uwezo wa viwanda kati ya China na Kenya litafanyika wiki ijayo mjini Nairobi, ili kuhimiza nguvu ya ushindani kwa uzalishaji wa viwandani nchini Kenya.

    Ofisa wa kundi maonyesho ya kimataifa la China Bw. Miao Ligang, amesema mjini Nairobi kuwa kwenye mkutano wa siku nne wa baraza hilo, wazalishaji wa Kenya watajifunza teknolojia mpya za kisasa za uzalishaji viwandani. Pia amesema makampuni ya China yako tayari kushirikiana na wenzao wa Kenya, kuhimiza nguvu ya ushindani ya bidhaa za Kenya.

    Mpaka sasa mashirika 81 yamethibitisha kushiriki kwenye baraza hilo, ikiwa ni pamoja na makampuni 12 makubwa ya China. Bw. Miao amesema hii itakuwa shughuli kubwa ya kwanza ya kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika, baada ya kufanyika kwa mkutano wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika mwezi Septemba hapa Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako