Shirika la ndege la Ethiopia ET jana lilizindua safari tatu za moja kwa moja kwa wiki kati ya Addis Ababa na Mogadishu, baada ya kusitishwa kwa miaka 41, hatua ambayo inaongeza kasi ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.
Akiongea kwenye sherehe ya uzinduzi iliyofanyika uwanja wa ndege wa Bole mjini Adis Ababa, naibu mkuu wa tume katika ubalozi wa Somalia nchini Ethiopia, Abdullahi Mohammed Warfa amesema kurejeshwa tena kwa safari hizo kutaisaidia jamii kubwa ya Wasomali wanaoishi nchi za nje kuunganishwa na nyumbani kwao.
Kuzinduliwa tena kwa safari hizo kumetokana na matarajio makubwa katika kanda hiyo pamoja na ziara ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed nchini Somalia mwezi Juni, yenye lengo la kuongeza kasi ya ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa kati ya pande mbili. Safari kati ya Addis Ababa na Somalia zilisitishwa muda mfupi tu baada ya mwaka 1977 na 78 kuibuka vita vya mpakani kati ya nchi hizo mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |