• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yajitahidi kutoa huduma bora za afya kwa wote

    (GMT+08:00) 2018-12-24 08:25:57

    Serikali ya Kenya mwaka 2018 imepiga hatua katika utoaji wa huduma za afya kwa wote na kwa gharama nafuu.

    Sekta ya afya nchini humo iko chini ya serikali za kaunti lakini pia ni mojawepo wa ajenda nne kuu za serikali ya kitaifa.

    Hadi sasa magavana na rais wa nchi hiyo, wameanzisha miradi kadhaa ya kufikisha huduma za afya kwa wananchi, Jacob Mogoa anaripoti kutoka Nairobi.

    Wakati akiapishwa kwa muhula wa pili kuwa rais wa kenya, Uhuru Kenyatta alitangaza ajenda nne kuu ambazo atatekeleza kwenye kipindi chake cha mwisho ofisini.

    Mojawepo wa ajenda hizo nne ni utoaji wa huduma bora na nafuu za afya kwa wote ifikapo mwaka 2022.

    Ili kufanikisha hilo, hatua kadhaa zimefikiwa ikiwa sasa baadhi ya serikali za kaunti zimepunguza malipo ya huduma za afya ama kuondoa kabisa malipo hayo.

    Kwa mfano hivi karibuni serikali ya kaunti ya Makueni ilifungua hospitali ya kina mama na watoto wachanga yenye vitatanda 200.

    Vitanda 120 ni vya kuwahudumia kina mama huku 80 vikiwa ni vya watoto wachanga.

    Profesa Kivutha Kibwana ambaye ni gavana wa kaunti hiyo anasema familia zote kwenye kaunti yake zinahitajika kulipa dola tano tu mara moja na kupata matibabu kwenye hospitali za serikali bila malipo zaidi.

    "Hii hospitali ya mama na watoto inachukua vitanda 120 watu wazima na 80 kwa watoto. Kwa hivyo nafikiri tumepiga hatua kazita kuendeelza matibabu hasa kwa kina mama na watoto. Na hii pia ni kuambatana na wito wa rais Uhuru Kenyatta ambaye alianzisha kmapeni ya huduma za afya kwa wote. Watu wakilipa dola tano watapata matibabu bila kulipa chochote"

    Na matunda ya uwekezaji kwenye sekta ya afya yanawafaidi wakaazi kama vile Jacqueline Wanza mwenye umri wa miaka 27 amabye anatumia kadi iliyolipiwa na familiwa yake kwa dola 5.

    "Hiyo kadi ndio inanisaidia kutoka mwezi wa Oktoba mpaka leo, sijalipa chochote kingine "

    Taakwimu za kitaifa nchini Kenya zinaonyesha kuwa ukosefu wa ajira ni asilimia 11.

    Hiyo ina maana kwamba asilimia hiyo 11 wanakabiliwa na changamoto ya kupokea huduma bora za afya kwani hawawezi kugharamia.

    Mpango wa kutoa huduma za afya kwa wote unalenga kuhahakisha watu kama hao hawakosi huduma hizo.

    Mwishoni mwa mwaka 2018, rais Uhuru Kenyatta aliongoza maafisa wa juu serikalini kuzindua mpango wa majaribio wa huduma za afya kwa wote.

    Kwenye hafla iliyofanyika mjini Kisumu, kaunti zinazolengwa kwa majaribio hayo ni kama vile Nyeri, Machakos, na Isiolo ambazo zina watu milioni 3.2 kwa jumla.

    Rais Kenyatta anasema kwenye uzinduzi huo kuwa serikali itatoa shilingi bilioni 3.1 za kufadhili mpango huo kwa jina Afya Care.

    "Kuanzia leo, wakenya wote kwenye kaunti hizo nne zilizoko kwenye mpango wa majaribio na ambao watakuwa na kadi ya Afya Care watapata huduma za matibabu bila malipo kwenye hospitali zote za serikali. Huduma za matibabu zitakazotolewa ni kama vile dharura, huduma za afya kwa watoto, huduma kwa waja wazito na waliojifungua, matibabu kwa wenye matatizo ya kiakili, maradhi ya kuambukiza na yasio ya kuambukiza na huduma za afya kwa jamii"

    Maradhi mengine ambayo yatafanyiwa ukaguzi na kutibiwa bila malipo ni kifua kikuu, HIV, na malaria.

    Juhudi za Kenya zimepata uungaji mkono kutoka kwa shirika la afya duniani WHO.

    Wakati wa uzinduzi wa mpango wa majaribio kwa kaunti nne mkurungezi mkuu wa WHO Tedros Adhanom alihuduria hafla hiyo, anasema.

    "Ningependa kueleza kwamba Shirika la afya duniani linaunga mkono mradi huu wa Kenya, tuko hapa kuwaunga mkono katika kila hatua, tukiwa na washirika kama vile benki ya dunia. Kwa amoja tunaunganisha mbinu zilizogawanyika na kutoa vipaumbele muhimu tukisaidiwa na wafadhili. Hatua mnazochukua sio tu zitabadilisha maisha ya mamilioni ya wakenya, lakini pia na mamilioni yaw engine katika kanda hii. Maazimio yenu ya hapa Kenya, ni sawa na aazimio yetu kwenu.Ngazi zote tatu za WHO zitaendelea kuwaunga mkono kwenye na safari hii."

    Ripoti ya benki ya dunia ya mwaka 2014 kuhusu sekta ya afya nchini Kenya inaonyesha kuwa ni asilimia 20 tu ya wakenya walio na bima ya matibabu.

    Pia sekta ya afya nchini humo mara kwa mara inakabiliwa na mgomo wa wauguzi, hali ambayo inahatarisha mamilioni ya wakenya wanaotegemea zahanati na hopitali za umma.

    Lakini mpango huu wa afya kwa wote unalenga pamoja na mambo mengine kuboresha mazingira na kufanya kazi kwa madaktari na utoaji wa vifaa vya kutosha.

    Mohamed Kuti ni gavana wa kaunti ya Isiolo ambayo ni mojawepo wa zile zinazofanyiwa majaribio ya mpango wa huduma za afya kwa wote, anaelezea jinsi mpango huo utakavyofanya kazi kwenye kaunti yake.

    "Sisi tumeweka maanani kuanza mpango wa huduma za afya kwa wote na kuhakikisha inafika katika maeneo yote ya mashinani. Tumefanya suhirikiano na shirika la living goods ambalo litaajiri wahudumu wa afya wa jamii wapatao 1,000 na kuwasambaza katika kila kona ya hii kaunti"

    Serikali ya Kenya inatarajia kuwa ifikapo mwaka 2022 kaunti zote 47 zitakuwa na huduma za afya kwa wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako