Kongamano hilo la Kimataifa liliandaliwa na Kenya kwa ushirikiano na Canada na Japan likiwaleta pamoja marais 11 na washiriki zaidi ya 4,000 ambao walijadiliana kuhusu ustawishaji wa uchumi wa majini.
Mwandishi wetu wa Nairobi Jacob Mogoa anaripoti kuhusu kongamano hilo ambalo ndio ilikuwa hafla kubwa zaidi ya kiuchumi nchini Kenya mwaka 2018.
Mwishoni mwa mkutano huo wa siku tatu, Viongozi na wajumbe, walikubaliana miongoni mwa mambo mengine kuimarisha uongozi wa kisiasa na ushirikiano wa kimataifa kupitia matumizi ya data na habari za kijasusi kudhibiti tishio la uharamia kuhusu rasilimali za maji na pia kujenga uwezo katika nchi masikini, kuendesha ufanisi zaidi kwenye mito, maziwa na bahari.
Kenya ikiwa mwenyeji wa mkutano huo ilitumia jukwaa hilo kubwa la kimataifa kuharakisha katika kufufua uchumi wake wa majini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lenye maudhui, "Uchumi wa majini na ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030", Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta limeipatia Kenya fursa ya kujadiliana na nchi mbalimbali kuhusu changamoto na jinsi ya kuboresha uchumi wa rasilimali za majini.
"Niko hapa kushirikiana nanyi, nina imani kwamba kwa ajili ya vizazi vyetu vya sasa na vijavyo, na uwezekano wa kuendelea kwa mazingira yetu tunafaa kutazama maisha ya baadae kwa njia tofauti ya mtazamo chanya wa uchumi wa rasilimali za majini"
Uchumi wa majini unamaanisha utumizi wa bahari,maziwa na rasilimali zake kwa ajili ya maendeleo endelevu ya uchumi.
Kwa njia moja ama nyingine nchi zote duniani zinafaidika na uchumi wa raslimali za maji.
Kwa mfao Uganda haijapakana na bahari lakini inatumia ziwa kubwa zaidi barani Afrika la Victoria kukupoea na kusaifirisha bidhaa kati yake nan chi jirani za Kenya na Tanzania.
Kwa kiasi kikubwa bidhaa zinazopitia kwenye ziwa la Victoria kwanza zinapitia baharini. Rais Museveni anasema anaona kwamba rasilimali ya uchumi wa bahari inafaa kutunzwa kwa hali na mali.
"Mpango wa Uganda katika suala hili,kwanza kabisa tumeanza kupiga vita uvuvi usio mzuri,bado tunatumia mbinu mbaya za uvuvi,lakini hivi sasa tunataka kuweka rada za kufuatilia wavuvi"
Makubaliano ya mwisho ya mkutano huu yanaendana na mahitaji ya nchi kama vile Somalia, ambayo hukabiliwa na tatizo la maharamia bali na kuwa na uwezo mdogo wa kiuchumi.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo anasema serikali yake itaendelea kuweka sera za kuhakikisha nchi hiyo yenye mojawepo wa pwani ndefu barani afrika inafaidika kiuchumi kutokana na bahari hindi.
"Uongozi wangu unatambua kuwa rasilimali hii kubwa ambayo bado haijatumiwa ipasavyo inaweza kuleta mabadiliko katika kushughulikia umaskini,uhaba wa chakula,uhaba wa maji,nishati ,na changamoto za ukosefu wa ajira"
Pia wajumbe walijifunza jinsi ya kupanua uvumbuzi wa kisasa,maendeleo ya kisayansi,na mbinu nzuri za kujenga mafanikio na wakati huo huo kuhifadhi maji kwa vizazi vijavyo.
Bibi Carole Kariuki ni mkurungezi wa chama cha sekta ya kibinafsi nchini Kenya.
"Kuna fursa nyingi ambazo ziko kwenye maji yetu na bado hazijatumika kikamilifu. Na bado hatujachukulia maji kama sekta kubwa ya kiuchumi. Lakini sasa ni wakati wa kuangalia jinsi ya kupata manufaa asilimia 100 kutokana na maji. Kwa mfano mara nyingi tunauza samaki wetu bila kuongezea ubora, lakini tunaweza kupata mapato zaidi tukiyaifadhi. Hivyo unafungua nafasi za ajira."
Zaidi ya wajumbe 4,000 na washiriki 32,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani, katika kongamano hilo la siku tatu walijifunza kuunganisha uwezo wa bahari, maziwa na mito ili kuboresha maisha ya watu wote,hususan walio katika mataifa yanayoendelea,wanawake na vijana .
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |