Ni mbio za ubingwa za Paris World mwaka wa 2003, za mita 5000. Wakat huo, Eliud Kipchoge ambaye alishinda mbio hizo alikuwa na umri wa miaka 18. Miaka iliyofuata, alizidi kutamba kwenye mbio hizo na kuweka rekodi kadhaa. Miaka 15 baadaye, Kipchoge ameingia kwenye vitabu vya kumbukumbu za riadha kuwa mkenya na mwanariadha wa pekee duniani kuwahi kuishi, kukimbia mbio za kilomita 42 kwa kutumia saa mbili dakika moja na sekunde 39. Akiongea na idhaa ya Radio China Kimataifa, Kipchoge anasema kwamba maandalizi murwa yalichangia yeye kuweka rekodi hii mpya ambayo wanasayansi wanasema kwamba, itachukuwa miaka mingi sana kuwahi kuvunja na mwanariadha wa kawaida. Je, siri ni ipi ambayo Kipchoge hutumia?
Nimekuwa kwenye coaching system nzuri. Nilikuwa na mpango mzuri na matayarisho mazuri. Nilikuwa nimejitayarisha vizuri.
Kila anapotoa hotuba zake, Eliud hakosi kumshukuru mkufunzi wake. Je, ana umuhimu gani katika ufanisi wake?
Mkufunzi wangu ndio kielelezo changu.
Ili kufaulu, mwanaridha anahitaji mtaalam ambaye atamwelekeza na kumpa mafunzo. Kipchoge anaelezea umuhimu wa mkufunzi kwa mwanariadha anayetaka ufanisi.
Kwenye mbio, hakuna mtu wa maana kubwa kama mkufunzi. Kocha ni kama mwalimu kwa mwanafunzi. Kocha anakuangalia wakati wa mazoezi. Jukumu lake kubwa ni kuhakikisha kwamba unaishi vizuri na una nidhamu ya hali ya juu.
Kipchoge ameiletea fahari nchi ya Kenya na haswa kaunti ya Uasin Gishu anakoishi. Alipoweka rekodi mpya yam bio za masafa marefu za Berlin za mwaka wa 2018, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na viongozi wengine kote nchgini, walimsifu na kumpongeza sana. Lakini, wanaojivunia zaidi ni wakaazi wa kaunti ya Uasin Gishu.
Ametuletea sifa sana. Tunampenda na tunaomba awakuze wengine.
Kipchoge ambaye anasema kwamba ndio mwanzo wa mambo. Wakenya watarijie mmengine makubwa. Kwa vijana, Eliud anawahimiza kutia bidii na kuamini ndoto zao.
Kwa vijana ni kwamba, tutiilie maanani riadha. Ni kama taaluma zingine.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |