Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi wiki hii mjini Addis Ababa alikutana na Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Bw. Workeneh Gebeyehu.
Bw. Wang amesema Ethiopia ni nchi yenye nguvu barani Afrika, inayoibuka na yenye fursa kubwa ya maendeleo. Pia amesema urafiki wa jadi kati ya China na Ethiopia unaendelea vizuri bila kujali mabadiliko ya hali ya dunia, na China iko tayari kuhimiza kuaminiana kisiasa, kunufaishana na kuungana mkono.
Kwa miaka 29 mfululizo waziri wa mambo ya nje ya China hufanya ziara yake ya kwanza ya kila mwaka barani Afrika, hatua ambayo Bw. Wang amesisitiza kuwa imekuwa ni desturi ya kidiplomasia ya China.
Lengo kuu la ziara hii ni kuwasiliana na nchi za Afrika kuhusu China inavyofuata kanuni za udhati, matokeo halisi, nia njema na kuzingatia haki wakati wa kutafuta maslahi ya pamoja, kama ilivyoelezwa na Rais Xi Jinping wa China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |