• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapanga kuanza kufundisha kichina mashuleni mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2019-01-08 09:29:36

    Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya mitaala ya taifa ya Kenya (KICD) Bw. Julius Jwan, amesema Kenya inapanga kuanzisha mafundisho ya lugha ya kichina kuanzia darasa la nne kwa wanafunzi wanaotaka kujifunza lugha ya Asia katika mwaka 2020, na lugha ya kichina itafundishwa kama lugha ya kigeni pamoja na Kifaransa, Kiarabu na Kijerumani.

    KICD imesema kuwa lugha ya Kichina inatakiwa kuzingatiwa nchini Kenya kwa sababu ni moja ya lugha zilizozungumzwa zaidi duniani kote.

    Bw. Jwan amebainisha kuwa Kenya pia itaweza kuvutia watalii zaidi wa China kama kukiwa na idadi kubwa ya watu wanaoongea kichina. Pia amsema watakaojifunza lugha ya kichina watakuwa na manufaa kwenye soko la ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako