Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezindua kituo kikubwa zaidi cha umeme wa kutumia jua katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati, ambacho kina uwezo wa kutoa megawati 20 za umeme.
Kituo hicho kiko katika wilaya ya Gomba, katikati ya Uganda, na tayari mradi huo umeunganishwa na gridi ya taifa na utatoa umeme kwa watu zaidi ya milioni 5 katika maeneo ya vijijini nchini humo.
Mradi huo unamilikiwa na David Alobo, ambaye mpaka sasa amewekeza dola milioni 24.5 za kimarekani katika mradi huo, na anatarajia kuwekeza dola milioni 200 za kimarekani kwenye miradi mingine minne kama huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |