Rais Edgar Lungu wa Zambia amefanya mabadiliko madogo kwa makatibu wakuu wa nchi hiyo, ambapo ameeleza kuwa hataongeza mkataba wa katibu wa Baraza la Mawaziri la nchi hiyo, Bw. Roland Msiska, unaomalizika tarehe 20 mwezi ujao.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya mawasiliano ikulu hapo jana imesema, rais Lungu amependekeza Bw. Msiska kuongoza Mamlaka ya Atomiki ya Zambia, ambayo ni taasisi mpya ya serikali, itakayokuwa na jukumu la kusimamia maendeleo ya miradi ya nyuklia nchini humo.
Nafasi ya Bw. Msiska itachukuliwa na aliyekuwa msaidizi wake, Bw. Patrick Kangwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |