Kampuni ya ndege ya Zambia jana imetangaza kusitisha safari kati ya mji mkuu ya nchi hiyo Lusaka na mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
Kampuni ya Proflight ya Zambia imesema, safari hizo zitasitishwa kuanzia tarehe 29 mwezi huu na zinatarajiwa kuanza tena tarehe 1 mwezi March mwaka huu.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo anayeshughulikia mambo ya serikali na viwanda Bw. Philip Lemba amesema, kampuni hiyo imechukua hatua hiyo kutokana na hali ya sasa nchini Zimbabwe, na changamoto inayokabiliwa nayo ya kurudisha fedha kutoka Zimbabwe.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |