Banda ya kikao cha faragha cha takriban saa saba, marais na waakilishi wa marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, walifika kwenye ukumbi wa Jumba La Mikutano La AICC. Kwenye kikao, mweneyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeondoka, ambaye pia ni rais wa Uganda, Yoweri Museveni alipokoze wenyekiti kwa Rais Paul Kagame kutoka Rwanda. Kwenye hotuba yake, rais Museveni alisisitiza umuhimu wa kuwa na mazingira murwa ya kufanyia kazi.
Swala la kuwepo mkataba wa soko huria kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na umoja wa Ulaya lilijadiliwa pia kwenye mkutano huo, pamoja na swala la michango ya nchi wanachama. Aidha kikao hiki pia kilijadili mswada wa kuwa na kura ya uwezekano wa kuundwa kwa viwanda vya kutengeneza nguo na viatu, ila wananchi wa mataifa ya Afrika Mashariki, waweze kupata bidhaa hizi kwa bei nafuu. Paul Kagame ni mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na Rais wa taifa la Rwanda.
Kwa miaka mingi, Afrika Mashariki imekuwa ikinunua magari yaliyotumika kutoka mataifa ya nje. Hivyo basi, kutatua swala hili, mswada wa utaratibu wa kuwepo kwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza magari hapa Afrika Mashariki, ulijadiliwa. Mswada huu ukipitishwa, hatua hii itapunguza gharama ya kununua magari yaliyotumika.
Maswala mengine yaliyojadiliwa ni kuondoa migogoro ya kibiashara haswa mipakani ili kurahisisha biashara kati ya raia wa Afrika Mashariki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |