• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 32 wa viongozi wa AU wamalizika Addis Ababa

    (GMT+08:00) 2019-02-12 07:50:09

    Mkutano wa kila mwaka wa viongozi na wakuu wa serikali wa nchi za Afrika umemalizika mjini Addis Ababa Jumatatu baada ya kujadili masuala ya mabadiliko ya taasisi za umoja huo, usalama na suala la wakimbizi. Kwenye mkutano huo, wa siku mbili, rais Paul Kagame wa Rwanda alimkabidhi uwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) rais Abdel Fatah el Sissi wa Misri aliyepokea zamu ya uongozi kwa mwaka mmoja .

    Kwenye hotuba yake ya ufungaji Al-Sisi ametoa wito wa kushughulikia ustawi wa watu wa Afrika na kusema katika mwaka mmoja ujao atajitahidi sana kufikia malengo yaliyowekwa na AU kwenye mkutano huo. Pia ametaja masuala mbalimbali ambayo atahakikisha yanafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na Kuanza kufanya kazi kwa Eneo la Biashara huria la Bara la Afrika AfCFTA, kujitahidi kufanya mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ukarabati wa wakimbizi na wakimbizi wa ndani na kutoa ajira kwa vijana.

    Viongozi kutoka mataifa 54 walikutana chini ya mada kuu ya mwaka huu ya Wakimbizi, wanaorudi nyumbani na wakimbizi wa ndani, IDPs, kwa lengo la kutafuta suluhisho la kudumu juu ya suala la kulazimika kuhama makazi barani afrika. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antony Guteres amesema mafanikio ambayo yamepatikana yametokana na jududi za pamoja za Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

    Juhudi za mageuzi katika utawala wa taasisi za AU na kuipatia kamisheni ya umoja huo nguvu zaidi ni kati ya mambo yaliyopendekezwa na Rais Paul Kagame alipokuwa mwenyekiti wa umoja huo. Wachambuzi wanasema mambo hayo yanajadiliwa ingawa kuna mvutano kati ya wanachama juu ya namna ya kutekeleza mageuzi hayo. Hata hivyo Kagame anasema ana matumaini kuwa tofauti zilizopo zitatatuliwa ipasavyo

    Huku hayo yakijiri mrithi wa Kagame Rais Abdel Fatah Sisi anaonekana atazingatia zaidi masuala juu ya usalama, kulinda amani na kazi za kukarabati baada ya vita, kutokana na hotuba yake ya ufunguzi. Sisi amesema lengo lake ni kuhakikisha Umoja wa Afrika unanyamanzisha bunduki kote barani Afrika ifikapo mwaka wa 2020.

    Kuhusu suala la mfumo Eneo la Biashara huria la Bara la Afrika, wachambuzi wanasema hiyo ingali ni changamoto kubwa kwamba tangu mataifa 44 kukubaliana juu ya mkataba wa kuanzishwa biashara huru barani humo, ni mataifa 19 tu yaliyokwisha idhinisha mkataba huo wakati inahitaji mataifa 22 kuweza kuutekeleza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako