Somalia na Umoja wa Mataifa zimezindua Mfuko wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Ujenzi wa Amani (PBF) ili kusaidia ujenzi wa amani nchini Somalia ukilenga zaidi miradi inayofanywa na serikali.
Naibu mwakilishi wa katibu mkuu na mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Bw. Peter de Clercq amesema, mfuko huo utaunga mkono miradi mitano mipya inayolenga utulivu, kuwasaidia wakimbizi wa ndani, maridhiano na mchakato wa ujenzi wa taifa, ardhi kwa ajili ya amani na uwiano wa wanawake katika ujenzi wa amani.
De Clercq amesema, kuna haja ya kuunga mkono juhudi za kuleta utulivu na maridhiano nchini Somalia kwa kukabiliana kwa pande zote na tatizo la wakimbizi wa ndani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |