• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Tanzania nchini China asifu ripoti ya kazi za serikali ya China

    (GMT+08:00) 2019-03-06 17:34:54

    Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki ameisifu ripoti ya kazi za serikali iliyotolewa jana na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang katika mkutano wa pili wa awamu ya 13 wa Bunge la Umma la China.

    Balozi Kairuki anaona sera ya kuweka kipaumbele katika ajira ya China inatilia maanani maisha ya wananchi wake na kupata mafanikio dhahiri, amesema sera hiyo inatambua kwamba, ajira ndiyo ni msingi wa utu wa raia wa China, na ajira ndio msingi wa kukua uchumi wa nchi hiyo. Amesema China itazidi kusonga mbele kwa kuweka mkazo kwenye suala la ajira na kuhimiza maendeleo ya uchumi.

    Balozi Kairuki pia alifuatilia mambo ambayo China itayaboresha ili kuvutia uwekezaji kutoka nchi za nje na kupanua upatikanaji wa soko, amesema katika hotuba hiyo, waziri mkuu wa China Li Keqiang ameeleza kwamba China itaondoa vikwazo vilivyowekwa ambavyo vinaathiri uwekezaji, na pia China itapunguza ushuru na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Amesema kuna mambo yaliyomo kwenye hotuba hiyo ambayo wamejifunza na watayapekea kwenye nchi zao ili kubadilishana uzoefu na kuiga mambo yanayoendana na mahitaji ya nchi husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako