• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya kazi ya serikali ya China yajadiliwa na wageni wengi

    (GMT+08:00) 2019-03-07 10:42:38

    Ripoti ya kazi ya serikali ya China iliyotolewa kwenye mkutano wa Pili wa Bunge la awamu ya 13 la Umma la China imetangaza kuwa China itashikilia kujiendeleza kupitia uvumbuzi, kufungua mlango katika pande zote, na kusukuma mbele kazi ya kupunguza umaskini. Mambo hayo yamejadiliwa na wageni wengi.

    Mwanasiana na msomi maarufu nchini Zimbabwe Bibi Fay King Chung amesema China inajizoeza na hali mpya, kuimarisha mageuzi kwa pande zote, na kuendeleza taifa katika sekta mbalimbali, mambo ambayo yametoa mfano wa kuigwa kwa nchi za Afrika.

    Anasema,"Dunia ya leo iko tofauti sana ikilinganishwa na ya mwaka 1949 na ya mwaka 1978, ambapo mabadiliko makubwa yametokea nchini China na dunia. China inaweza kutunga sera zake kwa mujibu wa hali mpya, hali hii inatia hamasa. Katika miaka ya hivi karibuni, China imefanya mageuzi mengi yenye ufanisi, kwa mfano katika sekta ya uchumi. Siku hizi, China inazingatia zaidi maendeleo ya teknolojia, ubunifu na kuboresha sekta ya uzalishaji kiviwanda."

    Bibi Fay anaona maendeleo ya China yametoa fursa muhimu kwa nchi za Afrika. Anasema, "naona China imehimiza maendeleo ya nchi za Afrika. Moja ni miundombinu kama vile viwanja vya ndege, barabara na madaraja, pili ni mawasiliano ya simu, kampuni kama Huawei imezisaidia sana nchi za Afrika. Aidha, uzalishaji kiviwanda katika nchi za Afrika uko nyuma, na China inaweza kutoa mchango katika sekta hiyo."

    Bibi Fay amesema kufuatia maendeleo ya ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ushirikiano kati ya China na Afrika utazidi kuimarishwa. Anasema, "Naona kutokana na manufaa ya pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', ushirikiano wa kikanda utakuwa mwelekeo mkuu wa maendeleo ya dunia. Mchakato wa utandawazi unaweza kukabiliwa na vikwazo, lakini ushirikiano wa kikanda na wa pande mbili utaimarishwa. China inaweza kufanya kazi kubwa katika kusukuma mbele ushirikiano huo, ukiwemo uwekezaji wake barani Asia, Afrika na Latin Amerika. Kuimarisha ushirikiano katika ujenzi wa miundombinu, nishati na biashara ilio kunanufaisha pande zote."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako