• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ajenda ya China ya usalama Afrika inashika kasi huku bara hilo likiendeleza juhudi za amani kwa ajili ya maendeleo

    (GMT+08:00) 2019-03-24 15:02:22

    Muda mfupi baada ya kuchukua hatamu za uongozi mwaka 2013, Rais wa China Xi Jinping alishinikiza kuwepo kwa sera dhabiti kuhusiana na mataifa ya kigeni na kusababisha viongozi wengi barani Afrika kuvutiwa na uhusiano wa karibu na Beijing, si tu katika ulimwengu wa biashara na mahusiano ya kiuchumi lakini katika masuala ya usalama pia.

    Katika hotuba yake ya kwanza kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2015, Rais Xi alizungumzia dhamira ya serikali yake ya kujenga ushirikiano dhabiti ambapo mataifa yanashirikiana kwa usawa, mashauriano ya pamoja na kudumisha maelewano. Hapa, alizungumzia umuhimu wa ushirikiano wa kiusalama kwa mapana katika hotuba yake.

    "Tunapaswa kujenga jukwaa la usalama unaoshirikisha usawa, haki, mchango wa pamoja na faida ya pamoja. Katika zama ya utandawazi wa uchumi, usalama wa mataifa unaingiliana na unaathiri kila mmoja." Rais Xi alisema.

    Kiongozi huyo wa China alisema bayana kuwa dunia inapaswa kuukumbatia mfumo wa pamoja wa kushughulikia kila aina ya vitisho vya usalama, ili kuzuia migogoro ambayo yamekuwa vikwazo kwa maendeleo. Alisisitiza kuwa hakuna taifa linayoweza kudumisha usalama kabisa kwa jitihada zake za kipekee.

    Ndoto hii ya kukuza usalama wa pamoja, wa kina, wenye ushirikiano na endelevu ni kile wengi wanaamini kuwa imeyafanya idadi kubwa ya mataifa barani Afrika kuelekeza macho yao Beijing.

    China tayari imezidisha juhudi zake za kupanua uhusiano wake na majeshi ya Afrika. Hii inadhihirika wazi kwani taifa hilo la pili kwa ukubwa wa uchumi duniani tayari limefungua kituo chake cha kwanza cha kijeshi Afrika nchini Djibouti.

    Itakumbukwa kwamba mwaka 2018, Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya China iliandaa mkutano wa usalama katika ya China na Africa jijini Beijing. Makamanda wa kijeshi 50 kutoka mataifa mabali mbali barani Afrika walihudhuria mkutano huo wa wiki mbili ambao ulikuwa wa kwanza kuwahi kufanyika.

    Kwa kuandaa kongamano hilo kubwa lililowalenga wakuu wa majeshi Afrika pekee, wachanganuzi wanaamini kwamba China iliweza kujidhihirisha kuwa mshirika mkuu wa bara hilo katika masuala yote ya maendeleo.

    Lakini hata kabla ya mkutano wa Beijing, idadi nzuri ya nchi za Afrika zimekuwa zikituma wajumbe kila mwaka kwa ajili ya mafunzo China. Inaaminika kuwa karibu kila taifa Afrika lina afisa wa ngazi ya juu katika jeshi ambaye amefanyiwa au kuendelea na mafunzo nchini China.

    Lakini kwa kukubali kusaidia kujenga uwezo wa vikosi vya usalama Afrika, wengi wanapendekeza kuwa China pia linaimarisha nafasi yake kama taifa linalotoa msaada wa ujuzi na utaalamu wa kiufundi katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja maswala ya ulinzi na kijeshi.

    Afrika kwa sasa inashuhudia ongezeko la uwekezaji kutoka kwa makampuni ya mataifa ya kigeni, na kupanuka kwa ushirikiano huu katika eneo la usalama linaonekana kuwadia kwa wakati mwafaka.

    SERA MPYA YA KIGENI YA MAREKANI

    Ama kwa kweli ushirikiano huu wa kiusalama umejiri wakati ambapo Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza mabadiliko katika sera za kigeni za nchi yake. Trump alifichua mwaka jana kuwa Marekani itapunguza bajeti ya kijeshi kuelekea Afrika hivyo kuacha bara hilo bila mshirika dhabiti katika suala hili.

    "Marekani haitatoa msaada kiholela barani Afrika tena bila kuzingatia mambo ya kuipa kipaumbele. Na, sisi hatuwezi tena kutoa msaada wetu kwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ambao hauna faida, ulioshindwa kufaulu na na usiyowajibika." Mshauri mkuu wa usalama wa Marekani John Bolton alisema.

    China kwa upande wake limesema kuwa kutokana na ushirikiano huo, China na Afrika yatajenga mtandao imara kwa kuleta kila mmoja katika meza ya ushauriano kwa masuala ya usalama. Hii ni pamoja na mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya vikosi kutoka pande zote mbili.

    Kwamba China ni taifa lenye uwezo mkubwa wa kijeshi si siri tena. Katika mchakato huu mzima, China itashiriki uwezo wake wa kijeshi katika silaha, na zana za kivita. Afrika bila shaka litafaidika pakubwa na utaalam wa kijeshi wa China ambayo matokeo yake ni kukita amani ambayo itakuza ustawi wa kiuchumi.

    Wengi wanaamini kuwa faida mojawapo ya ushirikiano na China katika Afrika ni uthabiti na mwendelezo wa sera. Mwenendo katika miaka 18 iliyopita imekuwa ile ya uthabiti wa ushirikiano na hatua kwa hatua yaonekena kuongezeka. Bila mabadiliko ya kisera uhusiano huu unajenga madaraja ya ushirikiano kati ya Afrika na China.

    Licha ya kupanua ushirikiano wa kijeshi na Afrika, sera ya China ya kutoingilia mambo ya ndani ya mataifa mengine imepongezwa. Hii hasa ni kwa sababu awali uwepo wa mataifa ya kigeni katika ardhi ya Afrika ilileta majonzo kwa wenyeji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako