• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha uokoaji cha China chasaidia kukinga maradhi nchini Msumbiji

    (GMT+08:00) 2019-04-01 17:01:18

    Kikosi cha uokoaji cha China kimefanya kazi katika eneo lililoathiriwa na kimbunga cha Idai nchini Msumbiji kwa wiki mbili. Licha ya ukoaji na matibabu, kikosi hicho pia kinafanya kazi ya kukinga maradhi katika sehemu zenye watu wengi haswa makazi ya watu walioathiriwa na maafa.

    Katika makazi ya Ifaba ya watu walioathiriwa na kimbunga cha Idai, waokoaji wa China wamepulizia dawa za kuua wadudu na vijidudu ili kukinga maradhi. Ofisa wa makazi hayo Bi. Georgina Fretto amesema, makazi hayo yana zaidi ya watu 1,100, ambao wamepewa chakula na huduma za afya, lakini kabla ya hapo, kazi ya kuua wadudu na vijidudu haikufanywa. Anasema,

    "tunahitaji sana huduma ya kuua wadudu, kwani kuna mbu wengi, zamani hakukuwa na watu waliokuja kufanya kazi ya kuua wadudu na vijidudu."

    Bi. Beatriz Garimbo anatoka eneo la Buzi ambalo limeathiriwa zaidi na kimbunga cha Idai, na alipoteza mume, baba na mama mkwe katika maafa haya. Sasa anaishi katika makazi ya Ifaba pamoja na binti yake mdogo. Anasema,

    "Nakishukuru kikosi cha uokoaji cha China kwa kutupatia msaada. Kazi yao ya kuua wadudu na vijidudu inaweza kukinga maradhi, na ni muhimu kwa sisi watu tunaoishi katika mahema."

    Mkuu wa kikundi cha kuwaua wadudu na vijidudu cha kikosi cha uokoaji cha China Bw. Fan Chaoyun, ambaye pia ni mtaalamu wa kinga ya maradhi ya kuambukiza, amesema makazi hayo yana watu wengi, na mazingira ya afya ni mabaya. Anasema,

    "baada ya kuingia kwenye makazi hayo, tuligundua kuwa kuna watu wengi, takataka zinatupwa bila kufunikwa, na vyoo ni vichafu. Hivyo tulipuliza dawa za kuua wadudu na vijidudu ili kukinga maradhi."

    Hivi sasa ugonjwa wa kipindupindu umetokea katika sehemu ya Beira, ambako idadi ya wagonjwa wa kuhara inaongezeka. Mtaalamu wa afya wa Msumbiji Bw. Albert Muanido, anaona kazi ya kuua wadudu na vijidudu itasaidia sehemu hiyo kuboresha mazingira ya afya. Anasema,

    "Naona tunahitaji huduma hiyo. Katika sehemu ya Beira, ugonjwa wa kipindupindu umetokea, na kuna wagonjwa wengi wa kuhara. Kazi ya kuua wadudu na vijidudu inasaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa."

    Licha ya makazi ya watu walioathiriwa na maafa, kikosi cha uokoaji cha China pia kimefanya kazi ya kuua wadudu na vijidudu katika ofisi ya Umoja wa Mataifa katika Uwanja wa Ndege ya Beira, na kwenye makampuni na makazi ya wachina nchini Msumbiji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako