• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalam kutoka Zambia ataka utayari wa kisiasa ili kutekeleza makubaliano ya biashara huria barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-05 19:38:20

    Mkurugenzi wa Biashara na Forodha iliyo chini ya Soko la Pamoja la Mshariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) Bw. Francis Mangeni ametoa wito wa utayari wa kisiasa kwa viongozi wa Afrika ili kutekeleza makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA).

    Makubaliano hayo yaliyosainiwa Machi 21 mwaka jana nchini Rwanda, yamefanikiwa kuridhiwa na nchi zinazotakiwa ili kuanza kutekelezwa baada ya Gambia kuridhia April Mosi mwaka huu.

    Bw. Mangeni amesema, kazi ngumu ya utekelezaji inaanza sasa, ambayo Afrika haina rekodi ya kujivunia, ameongeza kuwa, uongozi wa wazi wa kisiasa na ushiriki chanya wa watu walio katika ngazi ya juu kunaweza kuleta matokeo yanayotarajiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako