China na Umoja wa Ulaya zaahidi kuhimiza mazungumzo ya makubaliano ya uwekezaji
Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, mwenyekiti wa Kamati ya Ulaya Bw. Donald Tusk na mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker Alahamisi wiki hii mjini Brussels waliendesha kwa pamoja mkutano wa 21 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya. Viongozi hao wamekubaliana kuhimiza mazungumzo kuhusu makubaliano ya uwekezaji kati ya pande hizo mbili kupata mafanikio ndani ya mwaka huu, na kufikia makubaliano ya kiwango cha juu ndani ya mwaka kesho. Kwenye mkutano huo, Bw. Li amesema China siku zote inatilia maanani Ulaya, kuunga mkono nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuchagua njia ya kuungana, na kujitahidi kithabiti kukuza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya pande hizo mbili. Ameongeza kuwa kufungua mlango kunaleta fursa kwa China na Ulaya, na ushirikiano wa pande hizo mbili unaleta ustawi kwa dunia nzima. Amesema China inapenda kushirikiana na Ulaya kuhimiza uhusiano kati yao kupiga hatua mfululizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |