• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uamuzi uliotolewa na WTO kwa ajili ya China hauashirii ushindi wa upande wowote

  (GMT+08:00) 2019-04-20 21:55:50

  Shirika la Biashara Duniani WTO tarehe 18 lilitoa uamuzi kuhusu ombi lililotolewa na Marekani mwezi Desemba mwaka 2016, la utatuzi wa mgogoro kuhusu usimamzi wa viwango vya ushuru kwa mazao ya ngano, mchele na mahindi ya China. Uamuzi huo unaona kuwa hatua ya China haiko wazi, na inakwenda kinyume na ahadi iliyotoa wakati wa kujiunga na WTO, lakini shirika hilo pia halikubaliani na ombi la Marekani kuitaka China kutangaza mpango wake wa viwango vya ushuru kwa bidhaa hizo.

  China siku zote inapendekeza migogoro ya kibiashara itatuliwe kwa kufuata taratibu za utatuzi za WTO, na mamuzi ya WTO yaheshimiwe na kutekelezwa. WTO kutoa uamuzi juu ya mgogoro huo kunaonyesha hadhi yake muhimu katika kulinda kanuni ya biashara ya pande nyingi, na wala haushirii ushindi kwa upande wowote.

  Mfumo wa biashara ya pande nyingi wenye kiini chake kuwa ni WTO, umekuwa nguzo kuu katika kuhimiza maendeleo ya biashara ya kimataifa na kujenga uchumi wa dunia ulio wazi. Miongoni mwao, taratibu za kutatua migogoro zinachukuliwa kama mahakama ya WTO inayoshughulika utatuzi wa migogoro ya kibiashara, ambayo lengo lake ni kudumisha uwiano wa haki na wajibu kwa nchi wanachama na kuhakikisha utekelezaji wa kanuni za WTO.

  Lakini taratibu hizo za kutatua migogoro ya kibiashara za WTO zimeathiriwa vibaya na hatua za upande mmoja na sera za kujilinda kibiashara za Marekani. Wakati huohuo, WTO pia inahitaji kwenda na wakati, kufanyiwa mageuzi na maboresho.

  Mgogoro kuhusu mazao ya kilimo kati ya China na Marekani, ni suala lingine linaloikabili China. China itatumia fursa ya kutatua migogoro ya biashara na nchi nyingine wanachama chini ya mfumo wa WTO, kurekebisha na kuboresha mfumo husika, na kuinua kiwango cha utekelezaji wa ahadi zake kwa WTO. Katika mchakato huo, China pia itajadiliana na nchi wanachama wa WTO kwa ajili ya kuhimiza kwa pamoja mageuzi ya WTO na kuimarisha mamlaka na ufanisi wake, ili kuliwezesha kulinda vizuri mfumo wa biashara huria na ya pande nyingi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako