• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifaa na teknolojia ya China vyarahisisha kazi za utafiti wa maji na samaki Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-04-26 09:40:03

    Katika mfululizo wetu wa ripoti za ushirikiano wa wasomi wa China na Afrika leo tunaelekea kule nchini Tanzania ambapo taasisi ya jiografia na limnolojia ya Nanjing kutoka China imesaidia ile ya utafiti wa uvuvi nchini humo kwa vifaa vya maabara na hiyo kuendeleza uchunguzaji wa ubora wa maji na samaki. Ronald Mutie anaripoti.

    Maji ya Ziwa Tanganyika.

    Nyumbani kwa zaidi ya aina 500 ya Samaki na pia tegemeo kwa nchi 4 kwa shughuli za usafiri. Likiwa ndio ziwa la pili lenye kina kirefu duniani, ziwa Tanganyika pia linasifika kwa kuwa na maji safi. Lakini hapa pia kuna changamoto za jinsi ya kuhakikisha maji haya hayachafuliwi na kemikali kutoka viwandani au shughuli za kilimo.

    Tafiri, yaani taasisi ya utafiti wa uvuvi nchini Tanzania ndio inayojukumika kufanya utafiti na kuchunguza kila mwezi hali ya virutumbisho maji na samaki waishio humo. Taasisi hii hata hivyo haingeweza kutekeleza kazi zake kikamilifu kutokana na uhaba wa vifaa.

    Lakini mwaka wa 2008, taasisi ya jiografia na limnolojia ya Nanjing kutoka China (Niglas) ilisaini makubaliano ya ushirikiano na Tafiri na kuanza kufanya utafiti kwa pamoja na kushirikiana kwenye uchunguzi kwenye ziwa Tanganyika na mito inayoingiza maji yake ziwani humo. Kutokana na ushirikiano huo utenda kazi wa tafiri uliimarika na pia kuwezesha taasisi hiyo kuhifadhi data yake. Dk Ismael Aaron Kimirei ni mkurungezi wa kituo cha Tafiri mjini Kigoma.

    "Hakujawahi Kuwa na taarifa za ufuatiliaji wa ubora wa maji katika ziwa Tananyika kwa kipindi kirefu zaidi ya kipindi hiki. Awli kulikuwa na miradi mingine lakini ya kiama 2 au 3 hadi 5 na hakukuwa na ufuatiliaji wa mara kwa mara. Lakini sisi tunafanya ufuatiliaji wa maji kwa karibu miaka 8 sasa na tunafanya kila mwezi. Kwa ushirikiano huu tulio nao na wachina ni kwamba data yote tunayokusanya ni mali yetu hapa Tanzania."

    Na baadaye mwaka wa 2010 Niglas iltoa msaada wa vifaa vya maabara, pamoja na mafunzo ya kufuatilia hali ya ubora wa maji katika ziwa. Tanashio Mbonde akiwa mtafiti kwenye taasisi ya Tafiri amenufaika moja kwa moja kutokana na ushirikiano huu.

    "Ni asilimia kubwa kwenye teknolojia hasa vifaa kwa sababu hapo nyumba vifaa vetu vilikuwa duni na hatukuweza kuchunguza kiwango cha ubora wa maji ambacho ni kizuri zaidi lakini sasa ukingia pale maabara utakuta kuna vifaa vingi ambavyo vimetolewa na China. Lakini pia wachina wametusaidia kwa kutupa njia fupi za kufanya uchuguzi. Unafika tu kweenye maabara na kuweka sampuli yako na baada ya dakika kumi unapata matokeo. Pia wachina wanapokuja hapa tunawapeleka kwenye maeneo mbalimbali ya ziwa letu na mito na wananufaika kwa kusoma zaidi."

    Ushirikiano wa Niglas na Tafiri sio tu kwenye kituo cha Kigoma lakini pia kwenye makao makuu mjini Dar es salaam. Hapa Niglas tayari imesaidia kununuliwa kwa vifaa mbalimbali vya utafiti na Niglas pia itasaidia kujenga maabara ya kisasa ili kuendeleza ushunguzi wa samaki kwenye bahari hindi. Bibi Mary Kishe ambaye ni mtafiti mkuu mwandamizi katika makao makuu ya tafiri anakaribisha ushirikiano huu akiutaja kuwa ukurasa mpya utakaonufaisha pande zote mbili.

    "Tulikuwa hatuna maabara hata wacha vifaa. Kulikuwa na chumba tu ambacho kimetengwa kuwa maabara lakini hatukukitumia kutokana na ukosefu wa vifaa. Lakini walipokuja wataalam wa Niglas walikikarabati kile chumba ili kiweze kufanana na maabara na pia wakanunua vifaa kama vile jokovu, darubini na vingine ili kusaidia kuangalia ubora wa samaki na mazingira yake."

    Kulingana na bibi Kishe Chini ya ushirikiano wa Tafiri na Niglas pia wanafunzi kutoka Tanzania wanapata msaada wa masomo kwenda kusomea China huku nao wasomo wa China wakijumuika na wenzao watanzania kuendeleza utafiti wa samaki na maji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako