• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • "Ukanda mmoja, njia moja" Pendekezo muhimu kwa dunia iliyo wazi zaidi

  (GMT+08:00) 2019-04-28 09:53:05

  Mkutano wa pili wa baraza la kimataifa la "ukanda mmoja, njia moja" umefungwa jana hapa Beijing, na baadaye taarifa ya pamoja kutolewa baada ya mkutano wa majadiliano wa viongozi.

  Viongozi na watu waliohudhuria mkutano huo wamesema wameahidi kuwa watahimiza ushirikiano wa kimataifa katika ngazi za kanda ndogo, kanda na ngazi ya kimataifa, kupitia njia za ushirikiano kama "ukanda mmoja, njia moja" na mikakati mingine ya ushirikiano.

  Ikilinganishwa na mkutano wa kwanza wa baraza la kimataifa la "ukanda mmoja, njia moja" uliofanyika mwaka jana, mkutano wa mwaka huu umefikia matokeo 238 ya kiutekelezaji, na kusaini miradi ya ushirikiano yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 64. Mafanikio makubwa kiasi hicho na ya kiwango cha juu kwenye sekta mbalimbali, ni ushahidi kuwa nchi nyingi zaidi zinajiunga na kuwa wadau muhimu kwenye juhudi za kutafuta kuunganisha dunia, kuwa na ushirikiano wa pamoja, maendeleo na kujiendeleza kupitia pendekezo la "kanda mmoja, njia moja"

  Lengo kuu la "kanda mmoja, njia moja" ni kuondoa vizuizi vinavyokwamisha maendeleo ya uchumi wa dunia, kuhimiza mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa dunia, na kuweka msingi kwa ajili ya kufikia maendeleo ya pamoja. China ikiwa ndio kinara wa pendekezo la "kanda mmoja, njia moja imekuwa ikipanua uagizaji wa bidhaa, kupunguza ushuru kwa bidhaa zinazoingizwa China kutoka kwenye nchi zilizopo kwenye pendekezo hilo, na imekuwa inapanua biashara ya huduma, na kuwa soko muhimu kwa nchi zilizopo kwenye ukanda huo.

  Ripoti ya utafiti uliofanywa na benki ya Standard Chartered ya Uingereza iliyopewa jina la "China: Ukanda mmoja, njia moja unaanza kuwa na sura kamili" inaonyesha kuwa taasisi mbalimbali za fedha kama benki ya dunia, benki za sera benki za biashara na mashirika ya bima sasa yanajiunga na pendekezo la "ukanda mmoja, njia moja". Ripoti hiyo pia imeonyesha matarajio kuwa "kutoa fedha za maendeleo" na benki za biashara vitakuwa na mchango mkubwa kwenye mahitaji ya "ukanda mmoja, njia moja".

  Licha ya mchango wake katika kuhimiza maendeleo ya uchumi wa dunia, washiriki wa mkutano huo wamekubaliana kuwa, ili kutafuta maendeleo kupitia pendekezo la "ukanda mmoja, njia moja" kuna umuhimu wa kuunda mkono ajenda ya maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa ya mwaka 2030, na kufuata kanuni zinazotambuliwa kimataifa , na vigezo na uzoefu unaofaa, ili kuweka uwiano kwenye maendeleo ya kiuchumi.. Wizara ya fedha ya China pia imetoa mpango maalum kuhusu kusimamia madeni, ili kuboresha usimamizi wa madeni kwa nchi zinazotumia fedha kutoka kwenye mpango huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako