Hadi kufikia Ijumaa mchana asilimia 91 ya kura zilikuwa zimeshahesabiwa Afrika Kusini huku chama tawala ANC kikiongoza mbio hizo za uchaguzi kwa asilimia 57.56 ya kura.
Chama cha upinzani Democratic Alliance DA kinachukua nafasi ya pili kikiwa na asilimia 20.81 ya kura na Economic Freedom Fighters EFF kikiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia 10.42. Wakati chama cha ANC kikiongoza, lakini kinaonekana kutoungwa mkono katika majimbo mengi, na EFF kikionesha kukua katika majimbo yote. Zoezi la kura limemalizika Ijumaa na tume huru ya uchaguzi inatarajiwa kutangaza matokeo rasmi leo.
Habari zaidi zinasema Umoja wa Afrika jana ulikiri kuwa uchaguzi mkuu wa Afrika Kusini ni wa amani, uwazi, jumuishi na kuaminika. Kwenye taarifa yao waangalizi wa uchaguzi wa umoja huo, wamesema tume ya uchaguzi imeandaa na kufanya uchaguzi kwa njia ya kitaalamu na uwazi na kulingana na sheria husika za uchaguzi nchini Afrika Kusini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |