Sasa tuelekee Magahribi mwa Uganda amabako wandishi wa habari katika aneo la Bunyoro wameamua kuchukua hataua ya kivitendo kuchagiza juhudi za serikali za uhifadhi nwa mazingira ambazo pia zimethaminiwa katika Malengo ya Maendelleo Endelevu (SDGS).
Wanahabari hao kutoka wilaya nane za Bunyoro wamepanda miti Zaidi ya 700 ikiwa sehemu ya harakati zao muhimu za kuadhimisha Siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, 2019.
Maadhimisho ya enoe yalicheleweshwa hadi 31 mweizi huu ili kukamilisha harakati zinazoweka bayana haki na majukumu ya wanahabari na wadau wengine katika utekelezwaji wa maendeleo endelevu.
Wakati wa uzinduzi wa zoezi la upanzi, amekuwepo Afisa wa rasili malsi asili wa wialay ya Buliisa, Benard Tugume na kukaribisha uitikio huu wa wanadidhi wa habari.
"Nawapongeza wanahabari wa Bunyoro kwa kuchangua suala la upanzi wa miti kama sehemu ya harakati zao muhimu za kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habariya mwaka huu.
Kama serikali tutaendelea kuunga mkono juhudi zote za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira katiak eno hili la Bunyoro ili kuhakikisha kwamba miti zaidii imepandwa"
Ameongeza kuwa juhudi Zaidi za upanzi wa miti zahitajika katika eneo hili ili kukabiliana na atahri za moja kwa moja za ukuaji wa viwanda katika sekta ya mafuta na shinikizo dhidi ya rasilimali asili kutokana na ongezeko la idadi ya watu.
"Harakati hii inaendana na mipango yetu adhimu ya uhifahdi wa mazingira kando na kuitikia changamoto ya uchafuzi wa miti unaondelea. Pia napaswa kusema kwamba shughuli zinazoendelea kuhusiana na uchimbaji wa mafuta katika eneo hili zitaathiri mazingira"
Naibu Mkuu wa Wahudumu wa umma wa Buliisa Roney Agondwa ndiye alizindua rasmi zoezi hili la mupanzi wa miti.
"Ninyi ndio hutupasha habari. Mfano nikiona gazeti, ni lazima nolisome ili kufahamu kulikoni?. Hivyo ninyi ni watu muhimu sana na hasa mnapokuja kungana nasi. Mnasaidia serikali kutekeleza wajibu wake wa ulinzi wa mazingira ambayo ni msingi wa kipato na maisha. Hebu nichukue nafasi hii kuzindua rasmi upanzi wa miti:
Michezo ya mipira wa miguu ya kirafiki na vikundi tofauti, kufanya usafi kwenye maeneo ya umma ni miongoni mwa harakati muhimu zinazofanywana na wanahabari wa Bunyoro mbele ya maadhimisho yao.
Mwenyekiti wa Chamacha Wanaabari wa Hoima (HMA), John Bosco Tugume anaeleza kwa nini wamechukua hatua ya kivitendo.
"Kuanza ni kwamba kama wanahabari tumegusua na uchafuzi wa mazingira na hatuwezi kukaa na kuangalia kinachoendelea. Tuliamua kutekeleza zoezi hili ili kuonyesha dhamira yetu kama wanahabari. Pili ni kuweka katika vitendo kile tunachohubiri kwnai hatuwezi kusalia tu tukingea hewani au kuandika habari za kuchafuliwa kwa mazingira"
Mamia ya wananhci akiwemo Mwenyekiti wa tarafa ndogo iliyoathirika Zaidi ya uchafuzi Peter Okechi walishiriki upanzi huu wa miti vamizi aina ya gravelia na terminalia. Ameeleza kuwa ukataji wa makaa, kilimo na ukataji wa mbao nimiongoni mwa harakati za kiuchumi zinazochochea uchafuzi wa mzingira.
Kulingana na ripoti ya Mamlaka ya Misitu ya Uganda (NFA) ya mwaka 2015, Uganda inapoteza angalao hekta 92,000 za misitu asili kila mwaka. Pia ripoti inaonya kuwa misitu ya asili itaangamia kabisa nchini Uganda iwapo uchafuzi hautadhibitiwa katika kipindi cha miongo moja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |