Baada ya kuweka vikwazo dhidi ya kampuni ya Huawei ya China, Marekani hivi karibuni imeikashifu kampuni ya DJI ya China, kuwa ndege zisizo na rubani zinazotengenezwa na kampuni hiyo zina hatari inayowezekana kuwepo na kutishia kuamua kama kuweka kampuni ya kutengeneza vifaa vya video vya usimamizi ya Hikvision ya China katika orodha ya marufuku na kuizuia kununua teknolojia kutoka makampuni za Marekani au la katika wiki kadhaa zijazo. Kabla ya hapo, wanasiasa wachache wa Marekani hata walidai kuwa kampuni ya CRRC ya China kushinda zabuni ya ubunifu wa subway mpya ya mji wa New York kutaleta tishio kwa usalama wa taifa wa Marekani. … ana maelezo zaidi.
Katika siku chache zilizopita, baadhi ya wanasiasa wa Marekani wamefanya mashambulizi makali dhidi ya makampuni ya sayansi na teknolojia ya China. Ingawa Marekani ikiwa nchi yenye nguvu kubwa zaidi duniani, inaongoza katika sekta za sayansi na teknolojia, mambo ya kijeshi na uchumi, lakini baadhi ya wanasiasa hawataki kuona maendeleo ya nchi nyingine na kuziruhusu kuipita Marekani katika baadhi ya sekta. Kupitia maendeleo ya miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, China imetimiza uongozi katika baadhi ya sekta za teknolojia. Makampuni ya Huawei, DJI, CRRCC na Hikvision ya China yanatambuliwa na soko la dunia kutokana bidhaa zenye sifa nzuri zaidi, teknolojia za hali ya juu na bei nafuu, huku usalama wa makampuni hayo ukipitia ukaguzi mkali wa nchi nyingi duniani ikiwemo Marekani.
Hivi sasa, wanasiasa wa Marekani wanaoshikilia "Marekani Kwanza" wameacha kanuni za kushindana kwa haki zilizokuwa kiburi chao, na kutumia vibaya nguvu ya nchi kutekeleza ukandamizaji wa kiteknolojia dhidi ya China. Lengo lao ni kuzuia maendeleo ya teknolojia ya China na kulinda umwamba wa Marekani duniani.
Kwa makampuni ya China yanayoanzisha shughuli katika soko la nchi za nje, ukandamizaji wa kiteknolojia ulioanzishwa na Marekani ni changamoto nyingine na mtihani mwingine, ambayo yatakabiliwa na athari katika muda mfupi. Lakini kwa kuk mbali, makampuni ya China yatatumia ukandamizaji huo kama fursa ya maendeleo na nguvu kubwa ya kujiendeleza. China itakayoendelea kujiendeleza katika mawimbi, ni jibu zuri zaidi kwa ukandamizaji wa aina mbalimbali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |