Katika juhudi zake za kuendelea kupambana na umasikini hasa katika maeneo ya vijijini, nchi zinazoendea ikiwemo, Tanzania zinaweza kuiga jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kufanywa na jimbo la Shaanxi nchini China hasa katika kukuza kilimo na sekta ya utalii.
Jimbo la Shaaxi ambalo lina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 205,600 na idadi ya watu zaidi ya milioni 38, kwa kiasi kikubwa limefanikiwa kuondoa umasikini kwa wakazi wake hasa katika mji wa Ningqian uliopo katika jiji la Hanhong.
Ningquan ni maarufu kwa kilimo hasa kutokana na ikolojia na jiografia yake pamoja na utalii. Mji huu umezungukwa na milima mirefu, yenye hali ya ukijani kwa mwaka mzima hivyo kurahisisha shughuli za kilimo na kuvutia watalii kutoka sehemu mbalimbali.
Katika sekta ya kilimo, mji huu unazalisha kwa wingi zao la chai hivyo kutoa nafasi za ajira kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo hasa wanawake.
Kiongozi wa wanawake wanaofanya kazi katika shamba hilo, Wang You Quan anasema upatikanaji wa shamba hilo ulitokana na juhudi za pamoja baina ya wanakijiji na wawekezaji ambapo wanakijiji waliokua wanamiliki maeneo na mashamba kuzunguka eneo la mradi walikubali kutoa sehem ya maeneo yao ili yatumike katika uzalishaji.
"Hii inaonesha umuhimu wa uhirikiswaji wa wananchi katika mipango an miradi ya maendeleo ambayo inalenga kuwaondoa katika lindi la umasikini," alisema.
Pia, kila familia iliyotoa maeneo yao kwa ajili ya mradi huo hupokea gawio la takribani yuani 7,560 (takribani Shilingi milioni mbili na laki sita za Tanzania) pamoja na kuruhisiwa kufanya kazi katika shamba hilo hivto kujiongezea kopato mara dufu.
"Baada ya uzalishaji na kuuzwa kwa chai yetu, kila familia yenye hisa katika shamba hili hupata mgao unaostahili, na zoezi hilo hua linaendeshwa kwa uwazi kabisa," aliongeza.
Sehemu kuwa ya chai hiyo inauzwa kwa njia ya mtandao maeneo mbalimbali ya nchi ya China.
Awali, Naibu meya mtendai wa jiji la Hanzhong Bwana Chen Xiaoyong alisema hatua zote zinazochukuliwa zinalenga katika kutimiza azma ya Rais wa jamuhuri ya watu wa China Xi Jinping katika kukomboa wachina kutoka katika umasikini.
"Badala ya kununua ardhi kutoka kwa wananchi, tuliona no bora tukiwaruhusu waunganishe maeneo yao na ya wawekezaji ili wote ka wapamoja wapate faida endelevu, na tutaendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa kutumia rasilimali zilizopo hapa ili kufanikisha azma hiyo," alisema.
Alisema, hadi sasa zaidi ya vikundi vya ushirika 1,100 vimeanzishwa vikihusisha vijiji 800 na kwamba wataiongeza mkazo katika sekta ya viwanda ili kuongeza thamani ya malighafi zinazozalishwa.
Kwa mujibu wake, nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zinaweza kuiga mfumo huu unaotumika hapa katika kukuza maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla hasa katika maeneo ya vijijini.
Kama Tanzania itajifunza kutokana na hatua zinazochikuliwa katika Jiji la Hanzhong, ndani ya jimbo ya Shaanxi, inaweza kupiga hatua kubwa katika kukuza maendeo vijijini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |