Serikali ya Uganda imewahakikishia watalii kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kufuatia mlipuko wa homa ya Ebola kuripotiwa nchini Uganda.
Waziri wa nchi anayeshughulikia utalii Bw. Godfrey Kiwanda, amesema maambukizi ya mtu mmoja katika wilaya ya Kasese ni tukio la mtu mmoja tu, kwa kuwa wanafamilia wote wa mtu aliyeambukizwa wamefuatiliwa.
Shirika la afya Duniani WHO limesema hakuna haja ya kutoa tahadhari ya kusafiri kwenda Uganda baada ya nchi hiyo kukumbwa na maambukizi ya mtu mmoja. Shirika hilo limesema watu wanatakiwa kujilinda. Vikundi vya wataalamu wa afya tayari vimetumwa na mlipuko wa Kasese utadhibitiwa.
Kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo wizara ya afya ya Rwanda imetoa tahadhari mpya, na kuwataka wanyarwanda wageni walioko Rwanda kwenda hospitali mara moja, pindi wanapokuwa na dalili zinazonana na za ugonjwa wa Ebola.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |