• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kutuma maafisa wa ngazi ya juu kwenye maonesho ya Changasha

    (GMT+08:00) 2019-06-19 19:40:27

    Waziri wa biashara wa Kenya Peter Munya amasema ataongoza ujumbe wan chi hiyo kushiriki kweye maonesho ya kwanza ya kiuchumi na biashara kati ya China na Afrika yatakayofanyika mjini Changsha katika mkoa wa Hunan nchini China.

    Kenya pia itaonyesha bidhaa mbali mbalikama vile chai na kahawa kwenye maonesho hayo ya kati ya tarehe 27 na 29 Juni.

    Ronald Mutie anaripoti kutoka Nairobi.

    Waziri Munya, kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Nairobi Jumatano amesema kuwa wakati wa maonesho hayo ya Changasha, serikali itatia saini makubaliano mbalimbali ya kukukuza biashara kati ya nchi hizo mbili.

    "Tutasaini makubaliano kati ya baraza la kuza nje bidhaa la Kenya na shirika la china la biashara ya mtandaoni yatakayowezesha bidhaa za Kenya kuonekana kupitia kwa mtandao nchini China. Baraza la maua nchini Kenya nalo litasaini makubaliano na Funfree international Trade ya kufungua kituo cha ugamvi wa maua ya Kenya nchini China."

    Waziri munya anasema kufunguliwa kwa kituo hicho kutawezesha Kenya kuuza moja kwa moja maua yake kwenye soko la china.

    Kiwango kikubwa cha maua ya Kenya hufika kwenye soko la China kwanza kupitia Uholanzi ambayo hununua bidhaa hiyo kwa bei nafuu na baadaye kuuuza kwenye masoko kote duniani kwa bei ya juu.

    Na mbali na maua pia Kenya inaonyesha bidhaa nyingine za kilimo kama anavyoelezea mkurugenzi wa baraza la kuuza nje bidhaa Peter Biwott.

    "Vipaumbele kwenye maonesho hayo ni miundo mbinu , kilimo biashar na uhamishaji wa teknolojia na Kenya itajifunza mengi kuhusu uendelezaji wa miundo mbinu yake kama vile bandari. Tunapeleka pia majani chai, kahawa, macadamia, parachichi na maua kwa sababu tutafungua kituo cha kusambaza maua huko China. Kutakuwa na watu kama 20 hivi wanaotoka kwenye sekta ya kibinafsi"

    Maudhui ya maonesho hayo ni ushirikiano wa kunifaisha kwa usawa pande zote mbili na kuhimiza ushirikiano wa karibu zaidi wa kiuchumi kati ya China na Afrika.

    Maonesho ya Changasha yanafanyika siku chache tu baada ya Shirika la ndege la China Southern kuzindua safari za moja kwa moja kati ya Nairobi na mji huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako