Rais Xi Jinping wa China amesema nchi yake itatimiza ahadi zote ilizotoa kwa Afrika kwa kushikilia kanuni za udhati, matokeo halisi, udugu na nia njema pamoja na wazo sahihi la thamani kuhusu urafiki, haki na maslahi ya pamoja katika uhusiano kati ya pande hizo mbili.
Rais Xi amesema hayo alipoendesha mkutano wa viongozi wa China na Afrika, uliofanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele wa kundi la G20 mjini Osaka, Japan. Pia amesema China inapenda kuhimiza jumuiya ya kimataifa kuongeza uwekezaji barani Afrika na kufanya ushirikiano na Umoja wa Mataifa na wenzi wake wa kimataifa barani Afrika, katika msingi wa kuheshimu nia ya Afrika. Ameongeza kuwa China itatetea maslahi sahihi ya Afrika katika majukwaa ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa, kuhimiza rasilimali husika zipendelee Afrika, kuhimiza Umoja wa Mataifa kuchangia pesa kwenye operesheni za Afrika kujilinda yenyewe na kufanya juhudi zisizosita katika kusaidia kutimiza amani ya kudumu, maendeleo na ustawi barani Afrika.
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri ambaye pia ni mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, rais Macky Sall wa Senegal ambayo ni nchi mwenyekiti mwenza wa sasa wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC upande wa Afrika, pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wamehudhuria mkutano huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |