• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Kenyatta azindua Taasisi ya mafunzo ya baharini mjini Mombasa

    (GMT+08:00) 2019-07-09 10:00:46

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jumatatu alizindua Chuo cha Mafunzo ya Baharini mjini Mombasa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya mabaharia nchini humo. Chuo hicho cha Bandari cha mafunzo ya masuala ya baharini kinatoa mafunzo ya kipekee ya ubaharia, na kimeanzishwa kama sehemu ya mageuzi ya sekta ya usafiri wa baharini. Kupitia chuo hicho, serikali ya Kenya inatarajia kuziba pengo kubwa lauhaba wa mabaharia waliohitimu nchini Kenya na katika kanda ili kukidhi mahitaji ya sekta inayoibuka ya uchumi wa majini. Pia chuo hicho kitatoa elimu ya juu na mafunzo kwa wanafunzi watakaofuzu vizuri, ambao watapata shahada za diploma na vyeti.

    Katika hafla ya uzinduzi wa chuo hicho, Kenya ilisaini mkataba na kampuni ya Mediterranean Shipping utakaosaidia Shirika la Kitaifa la Meli la Kenya kusimama upya baada ya kuporomoka miaka mingi iliyopita. Mkataba huo pia utatoa fursa za ajira takriban 3,000 kwa vijana wa Kenya kila mwaka pamoja na nafasi 1,500 kwa vijana wa Kenya kuhudumu katika meli.

    Rais Kenyatta pia alisistiza kuwa mkataba huo utafanya Shirika la Kitaifa la Meli la Kenya kuweza kuingia katika bandari 500 duniani. Amesema kufufuliwa kwa Shirika la Kitaifa la Meli la Kenya (Kenya Shipping Line) kwa ushirikiano na Shirika la Mediterranean kutaimarisha uchumi wa taifa kupitia sekta ya bahari. Rais Kenyatta jana aliwapatia shahada mabaharia 62 na kuongeza idadi ya mabaharia waliohitimu hadi 78 na kati ya mabaharia 119 walioajiriwa na shirika la meli la Mediterranean ambalo ni mshrikia mkuu wa Kenya National Shipping Line,hadi sasa 40 kati yao wameshapatiwa meli za kuhudumu na kampuni hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako